idd

We provide better service

Wednesday, August 3, 2022

UKATILI WA KIJINSIA NA AINA ZAKE

 


UKATILI WA KIJINSIA NA AINA ZAKE

Ukatili wa kijinsia ni nini?

Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa uhuru, iwe hadharani au kwa kificho (TAMWA, 2017).

Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi (WiLDAF, 2016).

Mpaka hapo tushaweza kufahamu kwa uchache ukatili wa kijinsia hivyo basi twende tukaangazie aina za ukatili wa kijinsia japo kwa uchache

AINA ZA UKATILI WA KUJINSIA

Ukatili wa kingono

Ukatili wa kingono ni pamoja na ubakaji, ubakaji ni udhalilishaji wa kingono na pia ni ukatili wa kijinsia. Mtu aliyebakwa hupata maumivu makali, huwa na msongo wa mawazo, hukosa kujiamini, huwa na hofu, huweza kupata maambukizi, na hujiona hafai katika jamii. Pia kushikwa maeneo ya sehemu za mwili bila ridhaa ni mojawapo ya ukatili wa kingono. Kufanya ngono bila kinga nayenyewe inaingia kwenye kundi hili la ukatili wa kingono.

 

Vishawishi na ulaghai

Vishawishi na ulaghai kwa watoto wa kike ni ukatili wa kijinsia. Umbali wa kwenda shuleni kwa wanafunzi ni tatizo kubwa, hasa kwa watoto wa kike.  Baadhi ya watoto hujikuta katika ushawishi na ulaghai hali inayosababisha kukata tamaa na kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata mimba na kuolewa katika umri mdogo.



Ukatili wa kiuchumi

Ukatili wa kiuchumi unahusisha utumikishaji wa watoto ili kujipatia kipato au vinginevyo. Pia huu ni ukatili wa kijinsia. Utumikishwaji wa watoto huwakosesha watoto haki zao za msingi, pia huwaathiri kisaikolojia na kimwili. Kutokuwa na sauti katika mali inayokuhusu pia ni ukatili ambao unaingia kwenye ukatili wa kiuchumi, kufanyishwa kazi kwa malipo kidodo ni ukatili wa kijinsia pia. Kuto ruhusiwa kumiliki mali inayokuhusu nao ni ukatili wa kijinsia. Vilivile, usafirishwaji wa wanawake na watoto pia ni ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

 




Ukeketaji 

Ukeketaji ni kitendo cha kuondoa au kukata sehemu ya uke. Ukeketaji husababisha maumivu makali ya kidonda, kutokwa na damu nyingi, kuzimia, maumivu ya kisaikolojia, kuziba kwa njia ya mkojo, kuchanika vibaya wakati wa kujifungua, kuchelewa kujifungua na kupata maambukizi ya magonjwa kama VVU, fistula, homa ya manjano na hata kifo.

 


Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii 

Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao haujajulikana vema kwa watu wengi. Ukatili huu huwakuta zaidi vijana wanaotumia vyombo vya habari vinavyohusisha mawasiliano ya kimtandao. Ukatili wa kijinsia kwa njia ya mitandao unapotekelezwa husababisha athari nyingi hasa za kisaikolojia. Mtu anayetendewa ukatili huu huwa na hofu, wasiwasi, hukosa amani na furaha na pia husononeka na kukosa kujiamini. Mara nyingine muathirika anaweza hata kujidhuru.

 


Kipigo kwa wanawake 

Kumpiga mwanamke ni aina nyingine ya ukatili wa kijinsia. Kipigo hujenga chuki, woga, visasi na uhusiano mbaya ndani ya familia. Inampasa mwanaume kuachana na tabia hizi. Na pia, wanawake watoe taarifa kuhusu vipigo.



Kutelekeza familia 

Kutelekeza familia ni ukatili wa kijinsia. Tabia hii husababisha chuki, maradhi na watoto kukosa haki zao za msingi. Jukumu la malezi ya watoto ni la wazazi wote.



Ukatili ni kitendo chochote ambacho matokeo yake yanaweza kuleta kuumizwa kimwili au kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na vitisho vya vitendo hivyo, kushurutishwa, kupokonywa ujuru pasipo kujali ni vitendo vilivyotokea katika uwazi ama katika hali ya kujificha.


1 comment: